HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI OKTOBA 01,2017


Magazetini leo Jumapili October 1,2017


























0 comments:

CHINA YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA BILIONI 29.4 KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO



SeeBait
Serikali ya China imeipatia Tanzania msaada wa Shilingi 29.4bilioni kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu, utalii wa kijiolojia na kuukarabati Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Makubaliano ya msaada huo yametiwa saini Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James, kwa niaba ya Serikali, na Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Gou Haodong.
Katibu huyo amesema 22.4bilioni zitatumika kujenga Chuo cha Ufundi Stadi-VETA wilayani Ngara mkoani Kagera.
“Fedha hizo zitatumika kujenga vyumba 19 vya madarasa, ujenzi wa karakana 9 za kutolea mafunzo ya elektroniki, ufundi bomba, useremala, ufundi uashi na upakaji rangi” amesema James
Ameeleza kwamba kiasi hicho pia kitatumika kujenga majengo ya utawala, mabweni, nyumba za walimu na miundombinu mingine itakayosaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwenye chuo hicho.
“Tunaamini kwamba msaada huo utakuwa sehemu ya kusaidia jitihada za Serikali za kujenga uwezo wa wataalamu wake watakaochangia kukuza sekta ya uzalishaji na hatimaye kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana nchini” amesema James
Katibu Mkuu huyo amesema China, itatoa 6.7bilioni kwa ajili ya kuukarabati Uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam.
“Katika makubaliano yetu ya msaada wa kuendeleza Uwanja wa Taifa wenye uwezo wa kuingiza watu 60,000, China itatoa msaada wa kiufundi na vifaa vya kisasa vya michezo na utaalamu katika usimamizi na ukarabati wa uwanja” Amefafanua James
Amesema kiasi kingine cha shilingi 300milioni zitatumika kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa kuanzishwa kwa aina mpya ya utalii ujulikanao kama utalii wa kijiolojia “Geopark Project” katika Hifadhi ya Taifa Ngorongoro, mkoani Arusha.
Alisema lengo la utafiti huo ni kuhakikisha kuwa Tanzania inanufaika na maajabu mbalimbali ya kitalii yaliyopo nchini ambayo hayajatumika kikamilifu kuvutia watalii watakaoongeza pato la Taifa
“Tanzania ina kila sababu ya kujifunza kutoka katika Hifadhi ya Kimataifa ya Jiolojia ya Jiaozuo ya Yuntaishan ya China, iliyoanzishwa mwaka 2000 ambayo inaongeza asilimia 37.2 ya watalii kila mwaka na huchangia asilimia 12 ya pato la Taifa la nchi hiyo”
Tangu miaka ya 1960 mpaka sasa nchi hiyo imeendelea kuisaidia Serikali katika ujenzi wa miradi mbalimbali ukiwemo upanuzi wa Chuo cha Polisi Moshi, Ujenzi wa Maktaba mpya katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Kwa upande wake Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Gou Haodong, amesema ujenzi wa Chuo Cha Ufundi Veta huko Ngara mkoani Kagera utaanza haraka kama ilivyopangwa.
Kuhusu masuala ya utalii wa kijiolojia katika Hifadhi ya Taifa Ngorongoro, amesema Tanzania ina bahati ya kuwa na vivutio vingi vya utalii lakini haijavutia idadi kubwa ya watalii kutoka China kuja kuvitembelea.
“Zaidi ya watalii milioni moja kutoka China wanatembelea nchi mbalimbali dunia lakini kati ya hao, Tanzania inapokea watalii 20,000 tu kila mwaka kutoka China, lakini kwa kuanzisha mradi huu, watalii wengi kutoka China watavutiwa kuja nchini kufurahia utalii wa miamba, mandhari nzuri, urithi wa dunia, na kutembelea hifadhi za Taifa” ameongeza Haodong
Akizungumzia masuala ya uchumi, Balozi huyo amesema hivi sasa China imekuwa mwekezaji mkubwa zaidi nchini Tanzania kwa kuwekeza kiasi cha Dola za Marekani 1.77bilioni na kukuza ajira nchini.
Ameitaja baadhi ya miradi mikubwa iliyowekezwa kuwa ni pamoja na mradi wa miundombinu ya mtandao (Tanzania ICT broadband backbone), Bomba la gesi la kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, mradi wa kuboresha miundombinu ya bandari ,barabara na madaraja.

0 comments:

WANAUME WA SAME KILIMANJARO WASHINDWA KUZAA KWA SABABU YA BANGI NA MIRUNGI

SeeBait
 Imeelezwa kwamba idadi kubwa ya wanaume hawana uwezo wa kuzaa kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya kwa muda mrefu ikiwemo mirungi na bangi huko Same, Kilimanjaro.
Kutokana na hali hiyo Mbunge wa Same Mashariki Naghenjwa Kaboyoka, amemwomba Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kuingilia kati ili kuokoa vijana.
Kaboyoka amesema wananchi wengi wanajishughulisha na ulimaji wa zao hilo bila kuogopa sheria hususan za mamba vunta na Gonja.
Amesema sababu ya ulimaji na utumiaji wa bangi na mirungi ni kutokuwepo kwa kituo cha polisi katika maeneo hayo.
Amesema ameshaongea na Waziri Nchemba ambaye na amemuahidi kujenga kituo cha polisi katika maeneo hayo
ili kupunguza ulimaji wa mirungi na bangi lakini ni mwaka sasa umeshapita.
“Nikiwa katika bunge la mwisho niliongea na Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani kwamba ulimaji wa mirungi, bangi pamoja na uhalifu ni mkubwa na unazidi kushika kasi katika tarafa hizo."amesema Kaboyoka
Kaboyoka amesema usafiri wa kwenda kuripoti matukio ya kihalifu ni changamoto ya usafiri ambapo basi linatoka saa nane usiku hadi kurudi kesho yake.
“Sasa fikiria wahalifu watapelekwaje ,na nani atenda kuripoti na basi linaloondoka sa nane, hivyo uhalifu unazidi kuongezeka kutoka na kwamba hakuna wakuwakamata”amesema Kaboyoka.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya hiyo,Sospeter Magonera amesema wanapinga vikali kilimo hicho cha mirungi kutokana na kwamba kipo kinyume na sheria za nchi.
“Kilimo hicho kinachangia kwa asilimia kubwa kuharibu nguvu kazi ya jamii pamoja na nguvu kazi ya Taifa hali ambayo inarudisha maendeleo ya taifa nyuma”amesema Sospeter
Hata hivyo,diwani wa kata ya mamba miamba, Michael Mauya amesema uvutaji wa bangi na utumiaji wa mirungi umechangia kwa asilimia kubwa vijana kuishiwa nguvu za kiume hali ambayo imechangia kupungua kwa idadi ya watoto katika tarafa hizo.

0 comments:

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AIBUA UPYA MJADALA WA ALIYEMTISHIA BASTOLA NAPE NNAUYE


Kauli ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba kwamba mtu aliyemtolea bastola hadharani Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye si askari wa Jeshi la Polisi imeibua upya mjadala kuhusu suala hilo.

Waziri Mwigulu alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Clouds baada ya mmoja wa wasikilizaji kutaka kujua kama mtu huyo aliyemtolea bastola Nape alikamatwa au hajakamatwa.

Baada ya kauli hiyo, wadadisi wa masuala ya kisiasa wametaka waziri Mwigulu ambaye Jeshi la Polisi liko chini yake kuueleza umma mtu huyo kama si askari ni nani au awachukulie hatua askari walioshindwa kumchukulia hatua mtu huyo.

Nape alikumbana na kadhia hiyo Machi 23 ikiwa ni saa chache kupita tangu Rais John Magufuli alipotangaza kumwondoa kwenye Baraza la Mawaziri akihudumu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Baada ya kuondolewa asubuhi, siku hiyohiyo mchana Nape alipanga kufanya mkutano na waandishi wa habari katika Hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam ambako alikuta zuio la vyombo vya dola na alipolazimisha alijikuta akitolewa bastola mbele ya waandishi wa ndani na nje akitakiwa kurudi ndani ya gari lake na asifanye mkutano huo.

Tangu kutokea kwa tukio hilo, kumekuwapo mijadala hasa ikilenga kujua kwa nini hatua hazichukuliwi kwa mtu huyo licha ya video na picha mbalimbali zinazomwonyesha akitoa bastola na kumnyooshea Nape zipo na zinasambaa mitandaoni.

Mjadala huo ulitua katika Bunge la Bajeti lililokutana Aprili na hata katika mkutano wa Bunge uliomalizika wiki tatu zilizopita mjini Dodoma, baadhi ya wabunge wakitaka suala hilo na matukio mengine yajadiliwe ndani ya Bunge jambo ambalo halikufanyika.

Spika wa Bunge, Job Ndugai alichukua uamuzi wa kuitaka Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama chini ya Mwenyekiti wake, Balozi Adadi Rajabu kulishughulikia suala hilo na taarifa yake ilikuwa isomwe katika mkutano huo wa Bunge lakini ilishindikana na inatarajiwa kusomwa Novemba.

Juzi, waziri Mwigulu ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi akijibu swali la msikilizaji kuhusu mtu huyo kukamatwa au la akisema: “Ninachofahamu aliyemtishia bastola Nape hakuwa polisi kama ambavyo ilidhaniwa.”
Alisema katika tukio kama hilo, wahalifu wanaweza kutumia nafasi hiyo kufanya watakavyo, lakini uchunguzi wa suala hilo unaendelea.

Jana, gazeti hili lilimtafuta Nape kutaka kujua maoni yake kuhusu kauli ya waziri Mwigulu ambaye alisema kwa kifupi: “Siwezi kuzungumzia hilo kwani sijaona… nikiona nitaweza kuzungumza.”

Itakumbukwa, Aprili 8 mwaka huu, Nape akizungumza jimboni kwake kwa mara ya kwanza tangu alipoondolewa katika nafasi ya uwaziri alisema hakuchaguliwa kwenda kuwa waziri bali kuwatumikia wananchi huku akitoa ushauri kwa Rais Magufuli.

“Namwomba Rais wangu, na huu ni ushauri tu, simlazimishi, ninampa ushauri na kumwomba… kwa sababu matendo haya yanamjengea chuki yeye na wananchi kwa sababu wanadhani yeye ndiye anaowatuma,” alisema.

Nape alisema, “Sasa ili Rais wangu asijengewe chuki lazima ajiondoe kwenye jambo hili na namna ya kujiondoa ni kuunda tume iende kuchunguza imletee ripoti nani yupo nyuma ya haya matendo ya kihuni.” 

Alisema, “Ili atenganishe CCM na matendo ya wahuni wachache wanaotumia dhamana waliyopewa kuumiza watu na kupoteza watu lazima tume iundwe iende ikatuletee ukweli, ngoja niseme hapa kwani si nipo nyumbani tu… kama nilitolewa bastola si ni sawa na kufa tu, basi nipo tayari.”

Atueleze ni nani
Rais mstaafu wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), John Seka akizungumza na gazeti hili kuhusu kauli ya waziri Mwigulu alisema inaashiria kwamba uchunguzi wa suala hilo la Nape umekamilika hivyo taarifa yake inapaswa kutolewa kwa wananchi.

“Kama waziri amesema si askari, anawajibu wa kusema ni nani, kwani ushahidi wa mazingira upo. Lakini kama hakuwa askari alikuwa ni nani, je, anaruhusiwa kumiliki silaha na je, alitumwa na nani kwa lengo gani,” alihoji Seka.

Alisema, “Na kauli hiyo ya waziri inaashiria uchunguzi umekamilika na kubaini kwamba si askari… nilitarajia jana (juzi) wangemuuliza pale kama si askari wa Jeshi la Polisi ni nani kwani kwa kauli hiyo uchunguzi unaonesha umekamilika.”

Alipoulizwa na gazeti hili kuhusu hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu alisema: “Siwezi kuyazungumzia masuala hayo katika simu, ‘next week’ nitakuwa bungeni Dodoma utanitafuta.”

Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) mstaafu, Ernest Mangu alisema, “Sina hiyo fursa, waulize walio kwenye nafasi hiyo.”

Alipoulizwa kwamba anaweza kutoa maoni yake na yakafanyiwa kazi ili huyo asiyejulikana akajulikana, Mangu alisema, “Kama watahitaji wataniuliza, wewe unaniuliza kama nani, hayo ni masuala ya kiutendaji.”

Polisi wawajibishwe
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRD), Onesmo ole Ngurumwa alisema kauli ya waziri Mwigulu inazua utata hasa ikizingatiwa Nape alizuiwa kufanya mkutano na aliyetoa bastola aliitoa mbele ya askari wakishuhudia.

“Kitendo cha yule kutoa silaha mbele ya askari tena na RPC Kaganda (aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda) alikuwepo na akaachwa inaonyesha wanamjua ni mwenzao, kama si mwenzao au hawamjui, ilikuwaje atoe silaha hadharani na wamwache bila kumchukulia hatua,” alihoji.

Ole Ngurumwa alisema, “Kama ndivyo, basi Mwigulu awachukulie hatua askari wake waliokuwepo wakati huyo asiyejulikana anatoa bastola kwani ni kosa kutoa silaha hadharani tena mbele ya askari.”

Kauli ya kwanza ya Mwigulu

Itakumbukwa Machi 24 ikiwa ni siku moja tangu Nape kunyooshewa bastola, waziri Mwigulu alitumia akaunti yake ya mtandao wa kijamii kuzungumzia sakata hilo akisema, “Mh. Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni Mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana record ya uhalifu.”

“Kitendo cha mtu kumtolea bastola, sio cha kiaskari, sio cha Kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa bastola mbele ya kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini,” alisema.

Alisema, “Nahusika na usalama wa raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP (Inspekta Jenerali wa Polisi) atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari, na kama ni askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake,” alisema.


0 comments:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 30,2017






























0 comments: