Lowassa, ndesamburo Wawaponza Makada wa CCM



SeeBait
Kivuli cha aliyekuwa mgombea urais wa Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa, Edward Lowassa na mbunge wa zamani wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (marehemu) vinadaiwa kuitesa CCM.

Habari kutoka ndani ya chama hicho katika wilaya za Moshi, Siha na Hai zinadai kuwa vivuli vya wanasiasa hao ndiyo kiini cha kufutwa kwa uchaguzi wa mwenyekiti katika wilaya hizo.

Wiki iliyopita, chama hicho kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole alisema mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), umefuta uchaguzi katika wilaya nne. Mbali ya wilaya hizo tatu za Mkoa wa Kilimanjaro, nyingine ni Makete ya Iringa.

Alisema sababu ya kufuta matokeo hayo ni kubainika kwamba wagombea waliojitokeza hawakuwa na sifa pamoja na kubainika kuwepo na viashiria hatarishi kwa chama hicho kikongwe nchini.

Kutokana na uamuzi huo, Polepole alisema wilaya hizo zitaanza upya mchakato wa uchaguzi katika ngazi hiyo. Taarifa zilizopatikana jana kutoka Moshi Mjini zimeeleza kuwa tayari makada kumi na moja walikuwa wameshachukua fomu.

Taarifa zilizovuja kutoka ndani ya chama hicho katika wilaya za Hai, Moshi na Siha, zinadai kuwa mojawapo ya ‘viashiria hatari’ ni uwepo wafuasi wa Lowassa na Ndesamburo waliojitokeza kuwania nafasi hizo.

Wagombea katika wilaya ya Moshi ni Christopher Lyimo, Alhaji Omar Shamba, Consolata Lyimo na Elizabeth Minde ambaye ni mwenyekiti aliyemaliza muda wake na anayetetea nafasi hiyo.

Habari hizo zimedai kuwa kikundi kimoja cha makada wa CCM, kilichotwaa majukumu ya maofisa usalama wa chama, kinadaiwa kumwaga sumu kuwa mmoja wa wagombea alikuwa kwenye payroll ya Ndesamburo.

Hayati Ndesamburo alikuwa Mbunge wa Moshi Mjini kwa vipindi vitatu (2000-2015) alipoamua kustaafu mwenyewe. Alifariki dunia ghafla mapema mwaka huu.

“Hicho kikundi kinaoongozwa na kada mmoja (jina linahifadhiwa) kinajifanya usalama na kusema, (anamtaja mgombea) alikuwa kwenye payroll ya Ndesamburo ambaye ni marehemu,”

“Hivi wewe unavyoona ana shida gani mpaka awe analipwa na Ndesamburo wakati akiwa hai? Ni siasa za kuchafuana na hicho kimetengenezwa na huyo kada na kundi lake,” alidai kada mwingine wa CCM.

Mbali na mgombea huyo, lakini mgombea mwingine kati ya hao wanne anatajwa kuwa “haaminiki”, lakini haikuelezwa sababu za kuwajumuisha wagombea wote hadi uchaguzi wao kufutwa.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Moshi Mjini, Priscus Tarimo alipoulizwa kuhusu uamuzi huo wa Nec alisema umekuwa ni changamoto kwao kwa sababu walishajiandaa kwa uchaguzi.

“Ni uamuzi wa vikao vya juu kutokana ni taarifa za kiusalama kwa hiyo sisi hatuna budi kuupokea na leo (jana) wanachama wetu wameanza kuchukua fomu upya. Tunaenda vizuri,” alisema Tarimo.

Tarimo alipoulizwa iwapo waliogombea awali na kuonekana baadhi yao hawana sifa na wana viashiria hatarishi wataruhusiwa kugombea tena, alisema wanaruhusiwa kwa sababu hawakuzuiwa.

Minde aliyemaliza muda wake, ambaye ni wakili kwa taaluma alipoulizwa jana kuhusu hatima yake alisema yuko nje ya Moshi lakini atarejea leo na atachukua tena fomu kuwania nafasi hiyo.

Mbali na wilaya ya Moshi, taarifa kutoka wilaya za Hai na Siha zinadai kiini cha kufutwa kwa uchaguzi wao, ni baadhi ya wanaowania kutajwa kumuunga mkono Lowassa 2015.

Habari hizo zimedai kuwa baadhi ya wagombea ambao ndiyo wenye nguvu na wanaoonekana watashinda uchaguzi huo, wanatajwa kuwa katika mtandao wa Lowassa wakati akiwania urais ndani ya CCM.

Mara baada tu ya Rais John Magufuli kuingia madarakani, alifanya mkutano wake wa kwanza ofisi ndogo ya CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam na kulalamikia uwepo wa makada wasaliti.

Aidha, tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2015, chama hicho kimekuwa kikitekeleza mkakati wake wa kujiimarisha na kuwaondoa makada waliokisaliti katika kinyang’anyiro hicho kilichokuwa na ushindani mkali.

Ushindani huo ulikuwa baina ya Dk Magufuli na Lowassa ambaye licha ya kuondoka CCM na kugombea kwa tiketi ya Ukawa, bado alikuwa na kundi kubwa linalomuunga mkono ndani ya CCM.

0 comments:

Benki ya Dunia yaikopesha Tanzania Bilioni 336



SeeBait
Benki ya Dunia (WB) imeipatia Tanzania mkopo wa Dola za Marekani 150 milioni sawa na Sh336 bilioni kwa ajili ya kusaidia uhifadhi wa mazingira na kukuza utalii wa asili katika maeneo ya mikoa ya kusini mwa nchi.

Fedha hiyo ilitolewa na Shirika la maendeleo la kimataifa la benki hiyo (IDA) kupitia mradi wa uhifadhi wa mazingira kwa ajili ya utalii (REGROW) baada ya kuidhinishwa wiki iliyopita.

Fungu hilo litakalotumika kwa miaka sita, kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana, litazinufaisha kiuchumi kaya takriban 40,000 zilizopo katika hifadhi kwa kuwa kutajengwa miundombinu na fursa mpya za kiuchumi kwa lengo la kuongeza usimamizi wa hifadhi za asili.

Mpango huo una lenga kukuza uhifadhi wa mapori ya Taifa, mbuga, maporomoko ya mto Ruaha na kupunguza mwingiliano wa kimakazi kati ya binadamu na wanyama pori.

Maeneo yatakayohusika na mpango huo ni Mbuga za Katavi, Kitulo, Mahale, milima ya Udzungwa, Mikumi na Ruaha, Pori la Selous, Mito inayopitiwa na bonde la ufa (Nyansa na Tanganyika) .

Kuhusu Mpango huo, Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa nchi za Tanzania, Malawi, Somalia na Burundi, Bella Bird alisema utalii ni eneo muhimu kwa maendeleo ambalo linaweza kuongeza ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa asilimia 10 ya pato la Taifa (GDP) kwa hesabu za mwaka 2015.

“Nchi hii imejaliwa wanyama wengi na vivutio vya asili lakini vinavyotambuliwa na kujulikana zaidi ni vile vya maeneo ya Kaskazini mwa nchi. Kuanza kuyajali maeneo haya ya kusini kutaongeza idadi ya watalii, hivyo kuongeza faida za kiuchumi,” alisema Bird.

Alisema Tanzania imefanikiwa kuongeza idadi kubwa ya watalii ndani ya muda mfupi kutoka watalii 500,000 kwa mwaka 2000 hadi watalii zaidi ya milioni moja kutokana na kuvitangaza vivutio vyake.

“Ukaichilia mbali sifa ya kutunza vivutio, Serikali inapata mapato na sekta hii hutoa ajira nyingi, mpaka sasa Tanzania ni zaidi ya watu 400,000 walioajiriwa katika sekta hiyo,” alisema Bird.

Kwa upande wake mtaalamu wa mazingira wa Regrow, Daniel Mira alisema endapo eneo hilo la kusini litafanywa kuwa maalumu kwa vivutio Tanzania itakuwa imejiimarisha katika utalii.

“Hata mapato yatakayokuwa yakipatikana yatakuwa na uwezo wa kuendeleza vivutio vya kipekee jambo ambalo litalifanya eneo hilo kuwa kitovu cha ukuaji wa kikanda na la mfano,” alisema Mira.

0 comments:

Rais Magufuli azungumzia Ndege za Bombardier Ikiwemo Iliyoshikiliwa Canada



SeeBait
Rais John Pombe Magufuli amefunguka na kuzungumzia juu ya ndege za Tanzania sita zilizonunuliwa na serikali ikiwepo Bombardier Q 400-Dash ambayo inashikiliwa nchini Canada na kusema ndege hizo zitawasili nchini mwakani 2018.

Rais Magufuli amesema hayo alipokuwa kwenye Mkutano wa 33 wa Jumuiya Ya Tawala za Mitaa (ALAT) ambao uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam, Rais Magufuli amesisitiza kuwa Tanzania inakosa watalii wengi kutokana na kukosa ndege.

"Tumenunua ndege sita ndege mbili zimeshawasili Tanzania, lakini ndege zingine ikiwepo Bombardier zitawasilia mwakani 2018 mwanzoni. Tunafanya haya kwa ajili ya kutengeneza Tanzania mpya, nchi ambazo zina ndege zake idadi ya watalii wanaoingia kwenye nchi hiyo ni kubwa zaidi, nchi yetu ni ya pili kwa kuwa na vivutio vingi duniani lakini idadi ya watalii wanaoingia ni ndogo kutokana na kukosa ndege zetu" alisema Rais Magufuli

Serikali ilikiri ndege mpya aina ya Bombardier Q-400 Dash 8 iliyonunuliwa na serikali ambayo ilipaswa kuingia nchini toka mwezi Julai lakini ikashindikana kufika kutokana na kudaiwa na kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd iliyozuia ndege aina ya bombardier Q400-Dash 8 iliyonunuliwa na Tanzania nchini Canada.

0 comments:

Afikishwa Mahakamani Kwa Kuandika Uongo Kuhusu Mazungumzo kati ya Tanzania na Kampuni ya Acacia


SeeBait
Mkazi wa Chato mkoani Geita, Obadia Kiko (41), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kusambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook kuhusu mazungumzo kati ya Serikali na wawakilishi wa kampuni ya Acacia.

Wakili wa Serikali, Leonard Challo amedai mahakamani kuwa Agosti 3, 2017 huko Chato Geita mshtakiwa huyo alifanya kosa hilo kupitia mtandao huo wa kijamii wa Facebook.

Challo ametoa madai hayo leo Jumanne mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri. Mshtakiwa huyo anadaiwa kusambaza maneno kuwa "Taarifa kutoka  kikao cha mazungumzo kati ya Serikali na wawakilishi wa kampuni ya Acacia kuwa wanasheria wa upande wetu wanashindwa kutafsiri baadhi ya vifungu vya sheria hadi kufikia kuomba msaada kwa wanasheria wa Acacia sasa huoni hivi ni vituko mwizi anakusaidia sheria haahaa haha."

Inadaiwa aliendelea kusambaza maneno kuwa, "mazungumzo bado yanaendelea lakini wanasheria wetu wamebanwa sana ukizingatia wale jamaa wana vielelezo vyote vya mikataba kiukweli tumuombe Mungu maana Serikali ikitaka kuvunja mkataba na Acacia gharama kubwa zitatuusu."

"Lakini pia kuendeleza uvyama utatugharimu saana, baada ya mh. Rais Magufuli angewashirikisha mawakili wasomi waliokwishaiva wakili Lissu, wakili Kibatara na Fatma Karume kwenye mambo ya umuhimu kama haya yeye kaleta uchama sasa itatugharimu .// Dicteta Magufuli mist go" . Maneno hayo yanadaiwa kusambazwa na mshtakiwa huyo kupitia mtandao huo wa kijamii wa Facebook.

Wakili Challo amedai kuwa maneno hayo yalikuwa na lengo la kupotosha umma.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, mshtakiwa huyo alikana na upande wa mashtaka ukadai kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Kwa upande wa Wakili Peter Kibatala anayemtetea mshtakiwa huyo aliomba mteja wake apatiwe dhamana na kwa masharti nafuu.

Wakili Challo alieleza kuwa hana pingamizi la dhamana.

Hakimu Mashauri alimtaka mshtakiwa huyo kuwa na wadhamini wawili wanaoamika ambao kila mmoja atasaini bondi ya Sh 5 milioni.

Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 16, 2017. Hata hivyo mshtakiwa huyo hakuwa na wadhamini.

0 comments:

Mbunge kijana asababisha Chuo Kikuu cha Nairobi kufungwa….kisa?




Chuo Kikuu cha Nairobi kimefungwa kwa muda usiojulikana kutokana na kinachodaiwa kuwa ukosefu wa amani katika chuo hicho kutokana na wanafunzi kukabiliana na polisi mara kwa mara wakiandamana na hivyo kuhatarisha usalama.
Taarifa ya seneti ya chuo hiyo imeeleza kuwa asubuhi ya leo walitoa tangazo kwa wanafunzi wa chuo hicho kuchukua mizigo yao na kuondoka kwenye maeneo ya chuo mpaka hapo uongozi wa chuo utakapo jiridhisha kukifungua chuo hicho tena.
Polisi waliingia chuoni walipokuwa wakikabiliana na wanafunzi waliokuwa wakiandamana kulalamikia kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa kiongozi wa zamani wa wanafunzi wa chuo hicho Paul Ongili, maarufu kama Babu Owino. Owino, ambaye kwa sasa ni mbunge wa jimbo la Embakasi Mashariki jijini Nairobi, alikamatwa baada ya kudaiwa kumtukana Rais Uhuru Kenyatta.

0 comments:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO OKTOBA 4,2017




Magazetini leo Jumatano October 4,2017


























0 comments:

MAGAZETI YA LEO OCTOBER 3


































0 comments: