Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga R.P.C
Benedict Michael Wakulyamba, amepiga marufuku Vigodoro ndani ya jiji
hilo kutokana na vitendo hivyo kuhamasisha uhalifu.
Akiongea ofisini kwake Kamanda Benedict
amesema miongoni mwa viashiria vya uvunjivu wa amani ni Vigodoro,
ambavyo vinatumika kukusanya vijana wenye umri mdogo wakijiandaa kufanya
uhalifu.
“Miziki ya kigodoro ni miziki ambayo
ukiangalia namna inavyochezwa na hata washiriki wake ni vijana ambao
wanatumia kama sehemu ya maficho kwaajili ya kufanya uhalifu”, amesema
R.P.C Benedict.
Hata hivyo Kamanda Benedict ameongeza
kuwa hakutakuwa na ruhusa yoyote ya kufanya Vigodoro katika eneo lolote
na wananchi wanatakiwa kulinda utamaduni kwa njia nzuri na sio miziki
inayovunja maadili.

0 comments: