Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter
Msigwa amepandishwa kizimbani leo Alhamis Septemba 28,2017 katika
Mahakama ya Mwanzo Mjini Iringa kwa madai ya kumtusi na kutishia kumuua
aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kitwiru, Baraka Kimata.
Mbali na Msigwa pia Diwani wa Viti Maalum, Selestina Johanes na dereva
wa mbunge huyo, Godi Mwaluka wamepandishwa kizimbani kwa kosa hilo.
Akisoma shtaka hilo Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo, Rehema Mayagilo
amesema kuwa mbunge huyo na washtakiwa hao wawili wanashtakiwa kwa madai
ya kumtusi na kutishia kumuua diwani huyo.
Hakimu Mayagilo amesema kuwa Msigwa na wenzake walitenda kosa hilo jana
saa nane mchana katika viunga vya Ofisi za Halimashauri ya Manispaa ya
Iringa.
Baada ya kusomewa shtaka hilo Msigwa na wenzake wamepata dhamana na kesi
hiyo imeahirishwa hadi Oktober 9 mwaka huu itakapotajwa tena.
0 comments: