BODI YA WADHAMINI YA SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) YATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA KATAVI
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Jenerali
Mstaafu wa Jeshi la Wananchi ,George Waitara akisalimiana na Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi ,Izumbe Msindai baada ya kuwasili na
wajumbe wa Bodi hiyo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Mtango Mtahiko
akizungumza mara baada ya kuwapokea wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya
TANAPA .
Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi,Izumbe Msindai akieleza jambo kwa
Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA wakati wakitembelea hifadhi
hiyo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Jenerali
Mstaafu wa Jeshi la Wananchi ,George Waitara akitizama Viboko katika
hifadhi hiyo.
Baadhi
ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)
wakichukua taswira ya viboko katika Hifadhi ya taifa ya Katavi
walipotembelea .
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Jenerali
Mstaafu ,George Waitara akizungumza na askari waliopo katika mafunzo ya
awali ya Uhifadhi katika kambi ya mafunzo ya Mlele iliyopo mkoani
Katavi.
Askari
waliopo katika mafunzo ya awali ya Uhifadhi katika kambi ya mafunzo ya
Mlele iliyopo mkoani Katavi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya
Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Jenerali Mstaafu
,George Waitara alipowatembelea.
******
Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ikiongozwa na
Mwenyekiti wa bodi Jenerali Mstaafu George Waitara imetembelea Hifadhi
ya Taifa ya Katavi kwa ajili ya kukagua utendaji kazi ambapo ilipata
fursa ya kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Hifadhi Izumbe Msindai.
Bodi imepongeza utendaji kazi katika Hifadhi ya Katavi hususani suala
zima la kupambana na ujangili na juhudi zinazofanywa katika kuongeza
idadi ya watalii hifadhini.
Aidha, Jenerali Waitara aliutaka uongozi wa hifadhi kuongeza jitihada
katika kukabiliana na changamoto za mifugo ambayo ni kubwa kwa Katavi na
pia alipongeza uongozi wa mkoa chini ya Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali
mstaafu Raphael Muhuga kwa ushirikiano mkubwa anaotoa kwa hifadhi katika
kupambana na mifugo hifadhini.
Mapema kabla, bodi iliweza kutembelea kituo cha mafunzo cha Mlele na
kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Kituo Mhifadhi Genes Shayo na kupata
nafasi ya kuongea na askari wapya wanaoendelea na mafunzo katika kituo
hicho.
Jenerali Waitara aliwataka askari hao kuwa na nidhamu, uwajibikaji,
bidii na uzalendo katika mafunzo yao na kuwa ni lazima waonyeshe kuiva
ili waweze kupambana vilivyo na changamoto ya ujangili katika Hifadhi za
Taifa nchini.

0 comments: