DIWANI AWAAMBIA LEMA NA NASSARI WAACHE KUTAPATAPA NI BAADA YA KUDAIWA KUHONGWA NA CCM

September 27, 2017, aliyekuwa Diwani wa Murieti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ ambaye sasa amekihama chama hicho, Credo Kifukwe amemjibu Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari kuwa madiwani waliohama chama hicho wamenunuliwa.
Hatua hiyo imekuja siku tatu baada ya Mbunge Nassari kudai mbele ya waandishi wa habari kuwa anao ushahidi alioukusanya kuwa madiwani wanaoihama CHADEMA na kujiunga CCM wanarubuniwa kwa rushwa.
Aidha, Kifukwe amesema kuwa Mbunge huyo hana ushahidi kwamba yeye na madiwani wengine walinunuliwa bali walichonacho ni ushahidi wa kutengenezwa tu.
“Ninao ushahidhi Madiwani wanaohamia CCM wananunuliwa” – MBUNGE NASSARI

Aliongea diwani huyo kuwa mimi nimehama chadema baada ya kuona kazi ambazo zilipaswa kufanywa na upinzani zinafanywa na Rais  kwa juhudi zake Rais ana kamata mafisadi kwa umahili wake anawawajibisha viongozi wakuu wa selikali bila kuwa na hofu ya kiitikadi 
Aidha alisema huu ni wakati wa kufanya kazi naungana na watanzania wote katika jitihada za kuiunga serikali ya awamu ya watano Watanzania tuwakatae wanasiasa wenye lengo la kuipotosha nchi yetu tumempata Rais mchapakazi basi na sisi tuchape kazi ili kujenga Taifa lenye kujitegemea

Share on Google Plus

0 comments: