NB-Siyo mwanamke aliyesababisha kifo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaizidizi Jonathan Shanna Warioba, ametoa onyo kali kwa wananchi wenye tabia za udhalilishaji kwa wanawake kuacha tabia hiyo mara moja huku akisema kwamba udhalilishaji umesababisha kifo.
Kamanda Shanna amelazimika kusema hayo
hayo wakati akitolea ufafanuzi juu ya tukio la mauaji ya mkazi wa Kijiji
cha Vilabwa Wilaya ya Kisarawe Imma Habibu ( 26).
Kwa mujibu wa Shanna Marehemu aliuawa
juzi majira ya saa mbili asubuhi wakati walipokuwa kijiweni na wenzake
baada ya kutokea ugomvi kati yake na Ramadhani Habibu (23) ambaye ni
ndugu yake, baada ya mwanamke mmoja ambaye anadaiwa kuwa na maumbile
makubwa (makalio) kupita, mbele yao.
Alisema baada ya mwanamke huyo kupita
mbele yao walianza mabishano ambapo marehemu alisema mwanamke huyo ana
makalio makubwa na Ramadhani alisema ni makalio ya kawaida sio makubwa.
Kamanda Shanna alieleza kuwa baada ya
mabishano hayo ndipo ulipozuka ugomvi hadi kufikia hatua ya Ramadhani
kumuua kaka yake kwa kumchoma kisu kifuani upande wa kuliana na
alifariki dunia akiwa njiani anapelekwa hosptali ya kisarawe.
Alisema jeshi la polisi linamshikilia
mtuhumiwa kwa kufanya mauaji hayo na kuwa atafikishwa mahakamani mara
moja na kuwa amekubali kuwa amefanya mauaji hayo.
Kufuatia,tukio hilo kamanda Shanna
aliendelea kutoa onyo kwa wananchi na vijana wanaoshinda vijiweni
kuacha tabia ya udhalilishaji hasa kwa wanawake na kuwa kufanya hivyo
ni kosa kisheria na kuwa kama kuna mtu aliyefanyiwa vitendo vya namna
hiyo atoe taarifa polisi na atafikishwa mahakamani.
"Wito kwa wale wanaokiuka haki za
binadamu kwa kumdhalilisha mtu waache mara moja, mfano kisheria hata
kumkonyeza mtu ni kosa la jinai hivyo unapaswa kufika polisi, na
tutamfuatilia kisha kumpeleka mahakamani" Kamanda Shana amefafanua
Pia kamanda Shanna ametoa rai kwa wanawake kuvaa nguo zinazositiri maungo yao ili kuepusha vishawishi na matamanio kwa wanaume

0 comments: