MAGAZETI YA LEO OCTOBER 3


































DAKTARI ALIYEACHA WAGONJWA NA KWENDA KULEWA POMBE APATWA BALAA

 

SeeBait
WAZIRI wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu amemwelekeza Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Dk Zainab Chaula kumchukulia hatua daktari wa Hospitali ya Wilaya ya Maswa, Laurent Biyengo aliyedaiwa kushindwa kuingia kazini na kwenda kunywa pombe na kusababisha wagonjwa kutopatiwa huduma.

Aidha, Polisi wilayani humo imethibitisha kumkamata na kumseka ndani daktari huyo kwa maagizo ya Mkuu wa wilaya hiyo, Dk Seif Shekalaghe. Hatua imefikiwa baada ya baadhi ya wagonjwa waliofika katika hospitali hiyo Septemba 27, mwaka huu saa 1:00 hadi saa 3:30 usiku kukosa huduma kutokana na kutokuwepo kwa daktari huyo wa zamu na kusababisha ujauzito aliokuwa nao Salome John kutoka na kuharibika wakati akimsubiri daktari huyo aliyekwenda kulewa.

Waziri Ummy ametoa maelekezo hayo kwa njia ya simu baada ya kupata taarifa hizo kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) kutoka gazeti hili(Habarileo) juu ya wagonjwa waliofika kupata huduma katika hospitali hiyo na kumkosa daktari wa zamu.

Wagonjwa waliopatwa na madhira hayo wakizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu walisema walifika asubuhi katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupata matibabu, lakini cha kushangaza daktari wa zamu hakuwepo.

Walidai licha ya wauguzi kuwepo, lakini walishindwa kuwahudumia hasa mjamzito, Salome John aliyekuwa akilia kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata kwa maelekezo kuwa taratibu haziruhusu ni hadi hapo watakapoandikiwa cheti na daktari hali iliyosababisha mgonjwa huyo ujauzito wake kutoka.

“Nilimleta mwanangu akiwa ana mimba mara baada ya kunieleza ya kuwa anahisi maumivu makali tumbo tulifika hospitali majira ya saa 1:30 usiku, lakini daktari hatukumkuta licha ya kuandikiwa cheti lakini tulibaki kumsubiri daktari lakini hakuonekana ilipofika saa 3:20 usiku maumivu yalimzidi binti yangu na wauguzi walikataa kutuhudumia hadi tumwone daktari na hatimaye mimba yake ikatoka,” alidai Suzana Kalumbilo ambaye ni mama mzazi wa Salome.

Kwa mujibu wao, baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya kwa wagonjwa waliokuwepo walichukua jukumu la kumpigia simu Mkuu wa wilaya, Dk Shekalaghe ambaye naye alichukua jukumu la kumpigia simu Mganga Mkuu wa Wilaya, Dk Jonathan Budenu.

Walisema Dk Budenu aliyefika muda mfupi baada ya kupigiwa simu na DC wake, alifanya jitihada za kupata daktari mwingine ambaye alifika na kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa waliokuwepo. 

Inaelezwa kwamba ilipofika saa 3:40 usiku ndipo Bihengo alipofika akiwa amelewa huku hajitambui na kuingia katika chumba cha daktari, lakini Mganga Mkuu wa Wilaya, Dk Budemu alimtoa na kumtaka asitoe huduma yoyote kutokana na hali aliyokuwa nayo.

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU OKTOBA 2,2017

SeeBait





























PROFESSOR JAY! Baada ya nyumba yake kupitiwa na bomoabomoa

Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ‘Professor Jay’ ni miongoni mwa mahanga wa zoezi la bomoabomoa linaloendelea ambalo linafanywa na TANROADS kuondoa nyumba zilizopo ndani ya hifadhi ya barabara ili kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro.

Baada ya tukio hilo, kupitia Instagram yake, Professor Jay alieleza namna alivyosikitishwa na zoezi hilo lililotokea wakati yupo kwenye majukumu yake ya kibunge kwenye Jimbo la Mikumi.
>>>”Mimi ni mmoja wa wahanga wa hili zoezi la kubomolewa nyumba zetu huku Mbezi Kimara Tarehe 29/9/ 2017. Jana nikiwa katika majukumu jimboni Mikumi Majira ya saa kumi mbili hivi jioni, nilitaarifiwa kwamba, watu wa Tanroads wakiwa wameambatana na grader mbili na magari mawili ya polisi (defenders) yenye askari waliokuwa na silaha mbalimbali za moto walikuwa wanabomoa nyumba yangu.
“(sijawahi kuumia kiasi hiki 😭) Nimesikitishwa sana jinsi Tanroads wanavyoweza kujichukulia maamuzi bila ya kujali mhimili muhimu wa Mahakama wametoa maagizo gani. 🤔 Na taratibu zilizotumiwa kubomoa nyumba yangu bila ya mimi na Tanesco kupewa taarifa saa kumi na mbili jioni (haukuwa muda wa kazi) na kubomoa huku Umeme ukiwa unawaka ni kitendo ambacho kwanza kina hatarisha maisha ya wabomoaji wenyewe, maisha ya familia yangu pamoja na majirani zangu , LIMENISIKITISHA zaidi.
“Nasema hivi kwasababu Tanesco wamenipigia simu baada ya masaa 24 au zaidi baada ya zoezi la kubomoa nyumba kufanyika kunitaarifu kuja kukata Umeme kabla ya ubomoaji huo, pindi nilipo waambia kwamba mbona nyumba IMESHABOMOLEWA kabisa na sijaweza kuokoa kitu chochote na hata hiyo meter yenu mnayoiulizia mkaitafute kwenye kile kifusi cha nyumba yangu kilichokusanywa kwa pamoja na watu wa Tanroads. Tanesco walishangazwa sana kuvunjwa nyumba yangu kwa taratibu hizo.
“Lakini naamini kila kitu kinatokea kwa sababu maalum. Nimejifunza kumtegemea Na kumshukuru Mungu kwa kila jambo. Na hili ni moja ya mitihani ya hapa duniani. Nimepokea na kumsikiliza Mungu ana mipango gani juu yetu katika familia yangu mbeleni. Tumelipokea na Naamini tutashinda 🙏🏻.”