HII HAPA SAA YA RAIA MWEMA KUFUGIWA

SeeBait
Serikali imesitisha uchapishaji na usambazaji wa gazeti la kila wiki la Raia Mwema kwa muda wa siku 90 kuanzia leo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi amesema leo Alhamisi kuwa agizo hilo pia linahusu toleo la mtandaoni.
Dk Abbasi amesema adhabu hiyo inatokana na toleo namba 529 la Septemba 27 hadi Oktoba 3 lililochapisha habari ya uchambuzi inayosomeka “Urais utamshinda John Magufuli.”
Mwenyekiti wa Bodi ya Raia Mwema, Jenerali Ulimwengu amesema wameambiwa sababu ya kusitishwa kwa gazeti hilo ni habari hiyo.
Ulimwengu amesema kwa sasa wanashauriana kuona ni nini cha kufanya.
Dk Abbasi amesema katika taarifa kwa vyombo vya habari kuwa, Serikali inasisitiza uchambuzi huo ni maoni ya Raia Mwema ya haki (fair comment), hata hivyo, kwa bahati mbaya, na nia ovu, makala hiyo ilisheheni nukuu za kutunga na zisizo za kweli zikimsingizia Rais John Magufuli.
Amesema gazeti hilo pia limewahi kuonywa kwa makosa mbalimbali.
Amesema nukuu za uongo, kutungwa na zenye nia mbaya zikidai Rais alipata kusema ni, “Suruali za zamani msizitupe, mtazihitaji baadae,” na “Watakaobaki Dar es Salaam baada ya mwezi wa saba watakuwa wanaume kwelikweli.”
Dk Abbasi amesema walipotakiwa kuthibitisha wapi iwe ndani au nje ya nchi Rais alipata kutoa kauli hizo, wahariri wa Raia Mwema waliomba muda ambao walipewa. “Wakarejea na kuthibitisha kuwa hawana ushahidi huo, wakakiri kosa na kuomba radhi.”
Mkurugenzi huyo amesema bado Serikali inaamini Watanzania wakiufanyia mzaha upotoshaji wa taarifa na uchochezi katika zama hizi za Tehama amani na utulivu uliopo kwa miaka mingi utapotea na kukaribisha maafa kama ilivyotokea kwingineko duniani.
“Serikali, katika uamuzi huu, uliochukuliwa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo Waziri wa Habari katika kifungu cha 59 cha Sheria ya Huduma za Habari Na. 12, 2016, imetoa adhabu ndogo tofauti na ukubwa wa kosa kwa kuwa wahariri wa gazeti hili hawakufanya tashtiti, wamekiri kosa,” amesema.
Dk Abbasi amesema kupitia hilo, wamejifunza mambo kadhaa kuhusu changamoto za kiwango cha weledi wa uandishi wa habari nchini kiasi cha kuwalazimu kutoa ufafanuzi wa kina kwa faida ya umma na tasnia yenyewe; kwamba uandishi ni taaluma adhimu na yenye haki na wajibu vinavyopaswa kufuatwa na si kufanyiwa dhihaka.

VIJANA WA JOSEPH YONA NMC BOKORANI LEO KUKIPIGA TENA

Wachezaji wa timu ya UVCCM  inayofahamka kwa jina la NMC BOKORANI iliyo chini ya ccm tawi la bokorani chini ya mwenyekiti wao Mh JOSEPH YONA leo wanaingia kucheza mechi yao ya pili baada ya kutangaza ubabe kati mechi yao ya kwanza kwa kuwacharaza mabao mawili kwa moja timu ya WAENDAO

Vijana hao wanaenda kutafuta tiketi ya lobo fainali katika ligi ya slim cup mtoni temeke

Picha ya pamoja kabla ya mchezo huo
Vijana wakipasha misuli ili kuwa kabili mtoni sokoni
Muda mchache kabla ya mechi kuanza


SERIKALI YALIFUNGIA GAZETI LA RAIA MWEMA

SeeBait


BODI YA WADHAMINI YA SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA) YATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA KATAVI


Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi ,George Waitara akisalimiana na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi ,Izumbe Msindai baada ya kuwasili na wajumbe wa Bodi hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Mtango Mtahiko akizungumza mara baada ya kuwapokea wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA . 
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi,Izumbe Msindai akieleza jambo kwa Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA wakati wakitembelea hifadhi hiyo. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi ,George Waitara akitizama Viboko katika hifadhi hiyo. 
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakichukua taswira ya viboko katika Hifadhi ya taifa ya Katavi walipotembelea .
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Jenerali Mstaafu ,George Waitara akizungumza na askari waliopo katika mafunzo ya awali ya Uhifadhi katika kambi ya mafunzo ya Mlele iliyopo mkoani Katavi.
Askari waliopo katika mafunzo ya awali ya Uhifadhi katika kambi ya mafunzo ya Mlele iliyopo mkoani Katavi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Jenerali Mstaafu ,George Waitara alipowatembelea.
******
Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ikiongozwa na Mwenyekiti wa bodi Jenerali Mstaafu George Waitara imetembelea Hifadhi ya Taifa ya Katavi kwa ajili ya kukagua utendaji kazi ambapo ilipata fursa ya kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Hifadhi Izumbe Msindai.
Bodi imepongeza utendaji kazi katika Hifadhi ya Katavi hususani suala zima la kupambana na ujangili na juhudi zinazofanywa katika kuongeza idadi ya watalii hifadhini.
Aidha, Jenerali Waitara aliutaka uongozi wa hifadhi kuongeza jitihada katika kukabiliana na changamoto za mifugo ambayo ni kubwa kwa Katavi na pia alipongeza uongozi wa mkoa chini ya Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali mstaafu Raphael Muhuga kwa ushirikiano mkubwa anaotoa kwa hifadhi katika kupambana na mifugo hifadhini.
Mapema kabla, bodi iliweza kutembelea kituo cha mafunzo cha Mlele na kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Kituo Mhifadhi Genes Shayo na kupata nafasi ya kuongea na askari wapya wanaoendelea na mafunzo katika kituo hicho.
Jenerali Waitara aliwataka askari hao kuwa na nidhamu, uwajibikaji, bidii na uzalendo katika mafunzo yao na kuwa ni lazima waonyeshe kuiva ili waweze kupambana vilivyo na changamoto ya ujangili katika Hifadhi za Taifa nchini.

ALIYESAMBAZA UJUMBE WA POLISI KUONEKANA HOSPITALI KWA TUNDU LISSU AFIKISHWA MAHAKAMANI


SeeBait
Mtu mmoja wa Kigamboni, amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kusambaza ujumbe katika mtandao kwamba kachero wa Usalama wa Taifa ameonekana jijini Nairobi karibu na hospitali aliyolazwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Mshtakiwa huyo Mbutusyo Mwakihaba (40), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shtaka linalomkabili mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa.
Wakili wa Serikali Janeth Magoho alidai mshtakiwa anakabiliwa na kosa la kusambaza taarifa za uongo chini ya kifungu namba 16 cha Sheria ya mtandao namba 4 ya mwaka 2015.
Janeth amedai Septemba 11, mwaka huu kupitia mtandao wa ‘WhatsApp’ mshtakiwa aliandika “Huyu ni Kachero wa Usalama wa Taifa anatambulika kwa jina la Jose anaonekana Nairobi karibu na hospitali alikolazwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu…Mwaxcheni mwenzenu”.
Mshtakiwa alikana kutenda makosa hayo, upelelezi wa kesi haujakamilika ambapo Hakimu Nongwa alikubali kumpa dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika watakaosaini dhamana ya Sh milioni tano kila mmoja ambapo mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti hayo na kurudishwa mahabusu hadi Oktoba 12, mwaka huu.

WAZIRI DKT. TZEBA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA MBOLEA DAR ES SALAAM

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tzeba akiongea na wadau wa Mbolea wa Tanzania alipofungua mkutano wao katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs) 
Mkuu wa Shirika la Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRA) kwa Tanzania, Rwanda na Uganda, Profesa Nuhu Hatibu (kulia) akimkabidhi Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tzeba zawadi ya kitabu wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wadau mbolea walipkutana jijini Dar es Salaam leo Septemba 28 2017. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wauza Mbolea Tanzania, Salum Mkumba na Mkurugenzi Mkazi wa Taasis ya Biashara za Mbolea Afrika (AFAP), Dkt. Mbette Mshindo. 
Mkurugenzi Mkazi wa Taasis ya Biashara za Mbolea Afrika (AFAP), Dkt. Mbette Mshindo akiongea na wadau wa mbolea wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wadau mbolea walipokutana jijini Dar es Salaam jana Septemba 28 2017. Kutoka (kushoto) ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wauza Mbolea Tanzania, Salum Mkumba, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tzeba na Mkuu wa Shirika la Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRA) kwa Tanzania, Rwanda na Uganda, Profesa Nuhu Hatibu. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Eng. Mathew Mtigumwe akitambulishwa kwa wadau. 
Wadau wa Mbolea wa Tanzania wakifuatilia mada katika mkutano wao Dar es Salaam. 
Wadau wa Mbolea wa Tanzania wakifuatilia mada katika mkutano wao Dar es Salaam. 
Wadau wa Mbolea wa Tanzania wakifuatilia mada katika mkutano wao Dar es Salaam. 
Mkuu wa Shirika la Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRA) kwa Tanzania, Rwanda na Uganda, Profesa Nuhu Hatibu akiongea na wadau wakati wa ufunguzi wa Mkutano walipokutana jijini Dar es Salaam Septemba 28 2017. Kutoka (kushoto) ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wauza Mbolea Tanzania, Salum Mkumba na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Biashara za Mbolea Afrika (AFAP), Dkt. Mbette Mshindo na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba. 
Wadau wa Mbolea wa Tanzania wakifuatilia mada katika mkutano wao Dar es Salaam. 
Wadau wa Mbolea wa Tanzania wakifuatilia mada katika mkutano wao Dar es Salaam. 
Wadau wa Mbolea wa Tanzania wakifuatilia mada katika mkutano wao Dar es Salaam. 
Wadau wa Mbolea wa Tanzania wakifuatilia mada katika mkutano wao Dar es Salaam. 
Wadau wa Mbolea wa Tanzania wakifuatilia mada katika mkutano wao Dar es Salaam. 
Wadau wa Mbolea wa Tanzania wakifuatilia mada katika mkutano wao Dar es Salaam. 
Wadau wa Mbolea wa Tanzania wakifuatilia mada katika mkutano wao Dar es Salaam. 
Wadau wa Mbolea wa Tanzania wakifuatilia mada katika mkutano wao Dar es Salaam. 
Mkuu wa Shirika la Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRA) kwa Tanzania, Rwanda na Uganda, Profesa Nuhu Hatibu (kushoto) akiteta Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Eng. Mathew Mtigumwe wakati wa ufunguzi wa Mkutano walipokutana jijini Dar es Salaam jana Septemba 28 2017. 
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tzeba (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam. 

Makubwa Haya: AMUUA MWENZAKE WAKIBISHANA KUHUSU MAKALIO MAKUBWA YA MWANAMKE



NB-Siyo mwanamke aliyesababisha kifo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaizidizi Jonathan Shanna Warioba, ametoa onyo kali kwa wananchi wenye tabia za udhalilishaji kwa wanawake kuacha tabia hiyo mara moja huku akisema kwamba udhalilishaji umesababisha kifo.



Kamanda Shanna amelazimika kusema hayo hayo wakati akitolea ufafanuzi juu ya tukio la mauaji ya mkazi wa Kijiji cha Vilabwa Wilaya ya Kisarawe Imma Habibu ( 26).


Kwa mujibu wa Shanna Marehemu aliuawa juzi majira ya saa mbili asubuhi wakati walipokuwa kijiweni na wenzake baada ya kutokea ugomvi kati yake na Ramadhani Habibu (23) ambaye ni ndugu yake, baada ya mwanamke mmoja ambaye anadaiwa kuwa na maumbile makubwa (makalio) kupita, mbele yao.


Alisema baada ya mwanamke huyo kupita mbele yao walianza mabishano ambapo marehemu alisema mwanamke huyo ana makalio makubwa na Ramadhani alisema ni makalio ya kawaida sio makubwa.


Kamanda Shanna alieleza kuwa baada ya mabishano hayo ndipo ulipozuka ugomvi hadi kufikia hatua ya Ramadhani kumuua kaka yake kwa kumchoma kisu kifuani upande wa kuliana na alifariki dunia akiwa njiani anapelekwa hosptali ya kisarawe.


Alisema jeshi la polisi linamshikilia mtuhumiwa kwa kufanya mauaji hayo na kuwa atafikishwa mahakamani mara moja na kuwa amekubali kuwa amefanya mauaji hayo.


Kufuatia,tukio hilo kamanda Shanna aliendelea kutoa onyo kwa wananchi na vijana wanaoshinda vijiweni kuacha tabia ya udhalilishaji hasa kwa wanawake na kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na kuwa kama kuna mtu aliyefanyiwa vitendo vya namna hiyo atoe taarifa polisi na atafikishwa mahakamani.


"Wito kwa wale wanaokiuka haki za binadamu kwa kumdhalilisha mtu waache mara moja, mfano kisheria hata kumkonyeza mtu ni kosa la jinai hivyo unapaswa kufika polisi, na tutamfuatilia kisha kumpeleka mahakamani" Kamanda Shana amefafanua


Pia kamanda Shanna ametoa rai kwa wanawake kuvaa nguo zinazositiri maungo yao ili kuepusha vishawishi na matamanio kwa wanaume